Friday, 14 August 2015

HESHIMA YA MWANADAMU

Heshima ya mwanadamu i ngali akiwa hai, akiwa na akili zake timamu, akiweza kuamua mambo yake mwenyewe. hapa ndipo mwanadamu hutofautishwa na mnyama kabisa. mwanadamu ana mahali pazuri pa kulala, anakula vizuri kuliko mnyama, utamadumi wake unabadilika siku hadi siku, kutoka ukale kwenda kwenye usasa. Lakini mwanadamu huyu kitu kimoja tu humfanya afanane na wamyama wengine. kitu hicho ni kifo.Zaburi 49:11-12 inasema wazi kabisa
Makaburi yao yatabaki kuwa nyumba zao za   milele,   makao yao vizazi vyote,        ingawa walikuwa na mashamba na kuyaita    kwa majina yao.  Lakini mwanadamu, licha ya utajiri wake,      hadumu,  anafanana na mnyama aangamiaye.  
Mwanadau huyu mwenye malingo ya kila namna, maisha yake ndiyo yameishia hapa, mwanadamu hana ujanja juu ya kaburi na mauti. Mwanadamu atafanya ugunduzi wa kila namna ili kuyarahisisha maisha laiki hana uwezo wa kufanya ugunduzi wowote ule ili aishi milelle, atafanya kila kituko lakini hana ujanja na kifo, siku kikifika kimefika. hana namna yoyote ile ya kukikwepa. NImewasikia majina ya wanadamu wengi maalufu waliowahi kuitikisa dunia yote, walioonekana kuwa na hekima nyingi, waliokuwa na busara, waliokuwa wakarimu na sifa za kila namna zuri na mbaya. lakini sifa zao hizo hazikuweza kuwawezesha kukikwepa kifo. Hapa ndipo mwandishi wa zaburi anafamisha maisha ya mwanadamu na mnyama. kwani kama vile mnyama apoteavyo ndivyo, ndivyo mwanadamu Zaburi 49:12 Lakini mwanadamu, licha ya utajiri wake,      hadumu,  anafanana na mnyama aangamiaye. Mali yake na utajiri wake hauwewzi kumwokoa, nguvu zake hazina nafasi, uzuri wake wote huishia kaburini, maisha yake ya kifahari aliyokuwa akiyaishi akiwa kwenye majumba mazuri ya starehe hayana nafaSI ya kuihifadhi maiti ya mwanadamu huyu. mamalaka yake yote haina uwezo tena, cheo chake na ufalme wake hauna nafasi baada ya kifo, cheo chake au ufalme wake huchukuliwa na mwingine. 

Ewe mwanadamu unayetumainia uhai wako, una nini cha kujivuna baada ya uhai wako kuchuchukuliwa? Una nini tena cha kueleza juu ya maisha yako baada ya uhai wako kuchukuliwa? Pole kwa sababu haujui! Yamefichwa mwiongoni mwa wenye hekima na busara.
Maishani mwangu nmesikia mashujaa wengi sana ambao waliopata kuishi hapa dunia hapa, naweza kusema kutokana na uchambuzi wangu kuwa ni wema na wazuri na wabaya lakini wote hawa walipotea katika kifo! Ni mwanadamu mmoja tu ambaye kaburi halikuweza kumhifadhi kabisa! Kuzimu kuliogopa kwa ajili yake! Unamfahamu mtu huyo? Labda hujawahi kumskia, au unamskia lakini huna taarifa kamili au unamfahamu kwa uzuri zaidi. Lakini leo nitakueleza kwa ufunuo kidogo juu ya mtu huyo. Huyu ndiye anaye funguo za uzima na mauti. Nakwamia ili uwe na hamu ya kumtafuta nina hakika ataukomboa uhai wako dhidi ya kaburi.

Mtu huyo ni Yesu Kristo, alikuja dunian akafa kwa ajili yetu ili sisi tukombolewe kutoka kwenye utumwa wa dhambi na siku ya tatu alifufuka +_(1 Wakorintho 15:1-8,)

Yohana 3:13-21 inazungumzia namna Mungu alivyoupenda ulimwengu (mwanadamu mwenye dhambi) akaamua kumtoa Kristo ili aje achukue hukumu yetu na dhambi zetu, tulipaswa kuhukumiwa kutokana na dhambi zetu. Maandiko haya yanaendelea kwa kusema kuwa NURU imekuja ulimwenguni lakini watu wamependa giza! Neno la Mungu linasema YESU KRISTO ni NJIA na kweli  na UZIMA. Hakuna njia nyingine, nyingine ni ubatili mtupu.

Uzima na maisha yako baada ya kufa upo mikononi mwa YESU, lakini uamuzi wa kuishi milele baada ya kufa unao wewe leo, ni pale tu utakapoamua kumkutabali na kumpokea YESU KRISTO  LEO KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO.


Warumi 10;9-10 inasema wazi kuwa kwa sababu ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana na kuamini moyono mwako ya kuwa Mungu alimufufua katika wafu utaokoka. kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki na kinywa hukiri hata kupata wokovu
Waraka wa kwanza wa Yohana 5;12 unasema yeye aliye na Mwana [YESU] anao huo uzima wa milele, asiye na mwana wa Mungu hana huo uzima .

Ni kiu yangu wote tuwe na YEU KRISTO ndani ya maisha yetu ili tuiepuke hukumu ya moto wa milele, jehanam ni pabaya mahali pasipofaa kabisa, hapana tumaini milele yote, ni mateso milele yote, ni giza na vilio milele yote! Hebu ikimbie jehanam ya moto aliyoandaliwa shetani na malaika zake na wale wasioitii kweli kwa  kumkubali  Yesu Kristo ili abadilishe mwenendo wako, maisha yako, ulevi wako, tamaa zako, wizi wako, chuki yako, uchawi wako, ushirikina wako, uzinzi wako, kiburi chako na dhambi nyingine ili uwe kiumbe kipya kabisa na uishi maisha matakatifu (2 Wakorintho 5;17)

Kama hujaokoka au kumpokea Yesu Kristo kama Bwana na mwakozi wa maisha yako sema maneno yafuatayo| kwa kuamini kabisa moyoni mwako;

Bwana Yesu Kristo, ninakuhitaji, mimi ni mwenye dhambi. Nimekubali kwamba nimejitawala maisha yangu mwenyewe, na kutengana nawe. Asante kwa kifo chako msalabani kwa ajili ya dhambi zangu na kwa kunisamehe zote. Sasa nageuka na kutubu. Bwana, nakuomba uingie ndani ya maisha yangu na kunitawala kabisa. Badili maisha yangu yawe kama upendavyo wewe. Amin

Baada kusema maneno hayo kwa imani, sasa umekwisha kuokoka, Yesu amekusamehe dhambi zako zote na umekuwa kiumbe kipya, tafuta kanisa wanalokiri na kuamini wokovu na kuzaliwa mara ya pili, mwambie mwamini wa kanisa hilo atakupa maelekezo ya kufanya. Mungu akubariki kwa uamuzi wako.