Sunday, 7 June 2015

MAISHA MAPYA KATIKA KRISTO

Kwanini tuzungumze kwa habari ya maisha mapya? katika hali halisi hatuwezi kuzungumzia hali ya upya kama hakuna kitu kingine ambacho kimepita au kitu cha zamani.

Hii ndiyo sababu kubwa ya kuzungumzia maisha mapya katika KRISTO YESU. kwa sababu ni maisha tofauti na maisha ya kale tuliyozoea. Maandiko yanasema  ...... 
Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. (2 Wakorintho 5:17)

Paulo anaeleza wazi kabisa juu ya maisha ya kale, yaani maisha tuliyokuwa tunaishi kabla ya kuokoka
Tito 3:3 .... Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovo na husuda, tukichukiza na kuchukiana.
Vilevile anaeleza juu ya maisha kabala ya kuokoka katika Waefeso 2:1-3. Hii ndo hali anayokuwa nayo mtu ambaye hajaokoka, maisha yake yanaendeshwa na mfalme wa dunia hii yaasi shetan, amedanganywa na kuambiwa hakuna maisha baada ya kifo, amedanganywa hakuna wokovu duniani, anadanganywa kuwa hakuna Mungu. Watu hao akili zao zimetiwa giza, zimetiwa ganzi, ni wajinga, wapumbavu kwa sababu ya kufuata tamaa za dunia hii!

Tutaendelea zaidi Mungu akitupa kibali.... Lakini kabla haujaokoka hebu soma vizuri na tafakari sana.

BADILISHA MAISHA, BADILISHA ULIMWENGU

Karibu katika blogi hii ili tuweze kushare chochote ktk JINA LA YESU. lengo kubwa ni kubadilisha maaisha kama Mkristo (maisha ya kufanana na YESU) kama asemavyo katiak Wakolosai 3:10. lazima utu wetu uwe tofauti na watu ambao hawamjui Mungu. Karibu kwa mchango wako.

Mitume 11 aliowaacha YESU KRISTO wakti anapaa walitosha kuupindua ulimwengu wote (Matendo 17:6) ndiyo sababu ya sisi  kufikiwa na NEEMA hii ya injili. Lakini kumbuka hili hawakuweza kuupindua uliwengu kwa nguvu zao, Matendo 1:4 anawaagiza wasitoke mpakaa wamepokea ile ahadi. je ni ahadi gan hiyo? Matendo 1:8 inatueleza kwa habari ya hiyo ahadi anasema ......Lakini mtapoeka nguvu, akiisha kuwaajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashaidi wangu katika Yerusalemu na katika uyahudi wote, na Samaria na hata mwisho wa nchi. Ahadi hii inakamilika katika Matendo 2:1-4. hapo ndipo kitovu cha mabadiliko ya kuubadilisha ulimwengu ambapo Mtume Petro anasimama kwa ujasiri ya kuinena kweli ya Kristo bila woga wowote na watu zaidi ya 3000 wakabadilisha maisha yao (Matendo 2:37-42).

kwa hiyo ni lengo la blog hii ni kuhakikisha kila aliyeokoka anayaupindua ulimwengu kwa kuhubiri injili sahihi ya YESU KRISTO ambao ni uweza wa Mungu ulitaeo wokovu bila haya kwa maana ni uweza wa Mungu uletao wokovu (Warumi 1:16), kwa msaada wa Roho Mtakatifu ambaye ndiye nguvu yetu.

Nakukaribisha sana katika kazi hii ya kubadili maisha yetu (kuishi kama YESU alipokuwa duniani) na kuubadili ulimwengu kwa kuyaiga maisha yetu ambayo ni mfano wa maisha ya YESU KRISTO