Hii ndiyo sababu kubwa ya kuzungumzia maisha mapya katika KRISTO YESU. kwa sababu ni maisha tofauti na maisha ya kale tuliyozoea. Maandiko yanasema ......
Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. (2 Wakorintho 5:17)
Paulo anaeleza wazi kabisa juu ya maisha ya kale, yaani maisha tuliyokuwa tunaishi kabla ya kuokoka
Tito 3:3 .... Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovo na husuda, tukichukiza na kuchukiana.Vilevile anaeleza juu ya maisha kabala ya kuokoka katika Waefeso 2:1-3. Hii ndo hali anayokuwa nayo mtu ambaye hajaokoka, maisha yake yanaendeshwa na mfalme wa dunia hii yaasi shetan, amedanganywa na kuambiwa hakuna maisha baada ya kifo, amedanganywa hakuna wokovu duniani, anadanganywa kuwa hakuna Mungu. Watu hao akili zao zimetiwa giza, zimetiwa ganzi, ni wajinga, wapumbavu kwa sababu ya kufuata tamaa za dunia hii!
Tutaendelea zaidi Mungu akitupa kibali.... Lakini kabla haujaokoka hebu soma vizuri na tafakari sana.
Ujumbe mzurii
ReplyDelete