Tuesday, 14 June 2016

MLANGO WA KUFAA, UNAOPINGWA

*MLANGO WA KUFAA, UNAOPINGWA*

*1 Wakorintho 16:9*
 *_kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wako wengi wanipingao_*

Hayo yalikuwa ni maneno Paulo akinena juu ya nafasi ya kuhubiri aliyekuwa amepewa jiji la Efeso. Lakini pamoja na kufunguliwa mlango huu wa kufaa wapo walioinuka kumpinga na si wachache, tazama Matendo 19:13 na kuendelea, utaona namna alivyopingwa.

✍🏾Mlango ni fursa ya kufanya kitu fulani, ni kibali, nafasi. Ni opportunity ya kufanya jambo fulani.

✍🏾 Kuna fusra nyingi ambazo tunazo hasa baada ya kuokoka, tofauti na walimwengu. Ipo milango mikubwa sana ya baraka ambayo tayari tumefunguliwa. Tena ya kufaa sana.

✍🏾 Yawezekana umefunguliwa mlango wa kufaa katika huduma za kuhubiri, kufundisha neno la Mungu, kuwatia moyo watu, kuwasaidia watu, kukirimu, kulijenga kanisa la Mungu kiroho. Lakini wapo wapingao huduma hizo.

✍🏾 Yawezekana umepata Mlango wa kufaa katika katika biashara, kilimo, biashara, kazi yako, Elimu yako, familia yako au chochote kile ambacho kuna fursa, ila wapo wapingao, vipo vizuizi vikubwa sana.

✍🏾 Hao wapingao au hivyo vikwazo havisababishwi na watu wa kazini kwako, rafiki zako, wazazi wako, wachungaji wako au washindani wako ila ni ibilisi awatumiaye kuziba huo mlango, yeye ndiye huwatumia kuleta vikwazo na kupinga kwa namna yoyote ile ili usifanikiwe. Hutumia mapepo ili kuharibu huo mlango.

✍🏾 Kazi yetu leo ni moja, ni kuwapinga na wale watupingao kwa Damu ya Yesu Kristo wa Nazareti _*nao wakamshinda kwa damu ya Mwanakondooo*      (Ufunuo 12:11). Kuwapiga wale wazibao na kuweka vizuizi ktk milango yetu, _*mpingeni shetani naye atawakimbia,  (Yakobo 4:7)*_

✍🏾 Shetani ndiye apingaye na kuzuia mafanikio yetu, _*milango yetu ya masomo, milango ya huduma, milango ya biashara, milango ya baraka tele, milango ya uponyaji, yeye ndiye anayezuia uponyaji na kutesa watu, yeye ndiye mkatishaji tamaa, mtia woga kwa watu, mvuruga ndoa*_.

✍🏾 Maadam tumejua haki yetu kuwa tunayo, kuwa tuna milango iliyo wazi ila inazuiwa na huyu aliyeshindwa, tutasimama na kumwendea kwa jina la Bwana kama Daudi alivyomwendea Goliathi, tutakata kichwa chake na kuwapa ndege wale, tumechoka huyu mwovu kuyatukana majeshi ya Bwana, maana wewe ni askari na familia ya Kristo lazima tuinuke na kushika nafasi zetu.

✍🏾Hata kama mlango wa kupata kazi au ajira unapingwa kuzuiwa, lakini ayefungua milango ya gereza, alikata minyororo ya Paulo na mapingu yupo sasa kuondoa vikwazo na makufuli na vitasa vya bandia alivyoweka shetani, maana ukiona mlango km umefungwa ujue ni kitasa au kufuli la bandia alimeliweka shetani, we tikisa kidogo na fungua ingia kwa jina la Yesu. Bwana atafungua milango ya kufaa ya kila namna kwa kadiri ya wito wako na kusudi lako ambalo ndo hapa duniani kwa ajili ya kulitimiza.

✍🏾 Kumbuka,  *_hautainuka na kumpinga huyu mpinzani na mzuiaji wa mlango wako bila silaha za Kiroho ambazo ni Neno la Mungu, Imani, sala, maombi, utayari wa huduma, haki na utakatifu, lazima ujikane, ujitenge na tamaa za dunia hii, kujitenga na walimwengu, na kuukataa uovu kwa gharama yoyote ile, hata kumwagika damu ( Waebrania 12:4) inasema hamjafanya vita hata kumwagika damu,  mkishindana na dhambi_*

✍🏾 INUKA MPENDWA, HATUNA MJI UDUMUO HAPA. Jikane na ujitwike Msalaba wake, hapo utaona haya yakitimia, utaona pingu za shetani ktk milango yako ya mafanikio ikifunguka. Kumbuka haufanyi chochote ila kupata baraka zaidi ya kumpa moyo wako Kristo, na kulikubali kulitii neno lake.

By Isaac Lwendela; Mkristo
0768183433; 0783184333.
isaaclwendela@gmail.com

Monday, 13 June 2016

SIMAMQ IMARA, USITIKISIKE

1 Wakorintho 15:58.

58 Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.

Bwana Yesu tunakushukuru tena kwa kutupa siku nyingine na wiki tena ili tutende kazi pamoja na wewe.

Ndugu  ni neema ya ajabu kuwa katika familia ya Mungu. Kwa kule tu kuokoka tumeingizwa katika familia yake Mungu. Tumefanywa watakatifu.

Maneno ya Mungu hapa yanatuasa ya _*kuimarika*_.

✍🏾Bwana akuwezeshe uimarike ktk masomo yako huku ukijitahidi kudumu ktk kusudi lake siku zote.

✍🏾Bwana akakuimarishe katika biashara yako, bila kulegalega, kaimarike zaidi ukijua kabisa katika yote umepewa kwanza kuutafuta ufalme wa Mungu na haki yake ili uzidishiwe zaidi, kwa hiyo biashara yako isikusonge ukashindwa kumtumikia Mungu, kasapoti kazi ya Mungu kwa mapato tako, katafute muda wa kumwabudu Mungu pamoja na kutingwa ktk Biashara hiyo, ukijua siku utakapokufa biashara haitakuokoa.

✍🏾 Mfanyakazi ofisini kwako Bwana Mungu wa mbinguni akakuimarishe pamoja na changamoto zako, ukatafute kusudi la Mungu, wafanyakazi wezako na wateja wakajue Mungu wa mbinguni bado ana wafuasi wake waaminifu, usiruhusu chochote kile ktk kazi kiharibu uhusiano wako na Mungu. Kataa kutumiwa na shetani, hubiri hapo ulipo akiwemo hata bosi, _kataa mahubiri ya kishetani ya kukwambia huwezi au utaonekanaje_

✍🏾 Katika kazi nyingine, familia na chochote ufanyacho kaimarike zaidi pia, zidi kuwa imara  ktk kila jambo. Usikubali kuwa palepale. Kataa mahubiri ya shetani ya kukukatisha tamaa. *Kataa*tangu sasa. _Sema shetani hauwezi, nitazidi kuimarika katika Bwana nikiitenda kazi yake siku zote_

✍🏾 Maandiko hayo yanasema pia tusitikisike siku zote tukitenda kazi yako, ndugu mpendwa *_tusitikisike_*  *_tukaitende kazi yake siku zote_*. Najua kutikiswa kupo ila usikubali kutikiswa, hata km majaribu yako ni makali km moto, hata kama adui zako wamesimama kinyume nawe. Unajua nini, kikubwa hapa ni *usikubali kutikisika ingawa kutikiswa kupo* yaani hata km shetani atajaribu kukutikisa mwambie hivi _hivi unaweza kuitikisa ngome ya Yesu, mwambie toka lini we shetani ukamtikisa Mungu, asipo kujibu mwambie nipo ndani ya ngome imara isiyoweza kutikiswa na chochote_.

✍🏾 Ila yooote haya maandiko haya yanatufarijikwa kutuambia *kazi yetu si bure ktk Bwana*. Simama na usonge mbele, tutalipwa tusipozimia moyo, anasema hakuna atendaye kazi pasipo ujira.

By Isaac Lwendela: Mkristo
0768183433; 0783184333.
isaaclwendela@gmail.com.
📚UBARIKIWE EWE SHUJAA📚