*MLANGO WA KUFAA, UNAOPINGWA*
*1 Wakorintho 16:9*
*_kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wako wengi wanipingao_*
Hayo yalikuwa ni maneno Paulo akinena juu ya nafasi ya kuhubiri aliyekuwa amepewa jiji la Efeso. Lakini pamoja na kufunguliwa mlango huu wa kufaa wapo walioinuka kumpinga na si wachache, tazama Matendo 19:13 na kuendelea, utaona namna alivyopingwa.
✍🏾Mlango ni fursa ya kufanya kitu fulani, ni kibali, nafasi. Ni opportunity ya kufanya jambo fulani.
✍🏾 Kuna fusra nyingi ambazo tunazo hasa baada ya kuokoka, tofauti na walimwengu. Ipo milango mikubwa sana ya baraka ambayo tayari tumefunguliwa. Tena ya kufaa sana.
✍🏾 Yawezekana umefunguliwa mlango wa kufaa katika huduma za kuhubiri, kufundisha neno la Mungu, kuwatia moyo watu, kuwasaidia watu, kukirimu, kulijenga kanisa la Mungu kiroho. Lakini wapo wapingao huduma hizo.
✍🏾 Yawezekana umepata Mlango wa kufaa katika katika biashara, kilimo, biashara, kazi yako, Elimu yako, familia yako au chochote kile ambacho kuna fursa, ila wapo wapingao, vipo vizuizi vikubwa sana.
✍🏾 Hao wapingao au hivyo vikwazo havisababishwi na watu wa kazini kwako, rafiki zako, wazazi wako, wachungaji wako au washindani wako ila ni ibilisi awatumiaye kuziba huo mlango, yeye ndiye huwatumia kuleta vikwazo na kupinga kwa namna yoyote ile ili usifanikiwe. Hutumia mapepo ili kuharibu huo mlango.
✍🏾 Kazi yetu leo ni moja, ni kuwapinga na wale watupingao kwa Damu ya Yesu Kristo wa Nazareti _*nao wakamshinda kwa damu ya Mwanakondooo* (Ufunuo 12:11). Kuwapiga wale wazibao na kuweka vizuizi ktk milango yetu, _*mpingeni shetani naye atawakimbia, (Yakobo 4:7)*_
✍🏾 Shetani ndiye apingaye na kuzuia mafanikio yetu, _*milango yetu ya masomo, milango ya huduma, milango ya biashara, milango ya baraka tele, milango ya uponyaji, yeye ndiye anayezuia uponyaji na kutesa watu, yeye ndiye mkatishaji tamaa, mtia woga kwa watu, mvuruga ndoa*_.
✍🏾 Maadam tumejua haki yetu kuwa tunayo, kuwa tuna milango iliyo wazi ila inazuiwa na huyu aliyeshindwa, tutasimama na kumwendea kwa jina la Bwana kama Daudi alivyomwendea Goliathi, tutakata kichwa chake na kuwapa ndege wale, tumechoka huyu mwovu kuyatukana majeshi ya Bwana, maana wewe ni askari na familia ya Kristo lazima tuinuke na kushika nafasi zetu.
✍🏾Hata kama mlango wa kupata kazi au ajira unapingwa kuzuiwa, lakini ayefungua milango ya gereza, alikata minyororo ya Paulo na mapingu yupo sasa kuondoa vikwazo na makufuli na vitasa vya bandia alivyoweka shetani, maana ukiona mlango km umefungwa ujue ni kitasa au kufuli la bandia alimeliweka shetani, we tikisa kidogo na fungua ingia kwa jina la Yesu. Bwana atafungua milango ya kufaa ya kila namna kwa kadiri ya wito wako na kusudi lako ambalo ndo hapa duniani kwa ajili ya kulitimiza.
✍🏾 Kumbuka, *_hautainuka na kumpinga huyu mpinzani na mzuiaji wa mlango wako bila silaha za Kiroho ambazo ni Neno la Mungu, Imani, sala, maombi, utayari wa huduma, haki na utakatifu, lazima ujikane, ujitenge na tamaa za dunia hii, kujitenga na walimwengu, na kuukataa uovu kwa gharama yoyote ile, hata kumwagika damu ( Waebrania 12:4) inasema hamjafanya vita hata kumwagika damu, mkishindana na dhambi_*
✍🏾 INUKA MPENDWA, HATUNA MJI UDUMUO HAPA. Jikane na ujitwike Msalaba wake, hapo utaona haya yakitimia, utaona pingu za shetani ktk milango yako ya mafanikio ikifunguka. Kumbuka haufanyi chochote ila kupata baraka zaidi ya kumpa moyo wako Kristo, na kulikubali kulitii neno lake.
By Isaac Lwendela; Mkristo
0768183433; 0783184333.
isaaclwendela@gmail.com
No comments:
Post a Comment