Monday, 13 June 2016

1 Wakorintho 15:58.

58 Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.

Bwana Yesu tunakushukuru tena kwa kutupa siku nyingine na wiki tena ili tutende kazi pamoja na wewe.

Ndugu  ni neema ya ajabu kuwa katika familia ya Mungu. Kwa kule tu kuokoka tumeingizwa katika familia yake Mungu. Tumefanywa watakatifu.

Maneno ya Mungu hapa yanatuasa ya _*kuimarika*_.

✍🏾Bwana akuwezeshe uimarike ktk masomo yako huku ukijitahidi kudumu ktk kusudi lake siku zote.

✍🏾Bwana akakuimarishe katika biashara yako, bila kulegalega, kaimarike zaidi ukijua kabisa katika yote umepewa kwanza kuutafuta ufalme wa Mungu na haki yake ili uzidishiwe zaidi, kwa hiyo biashara yako isikusonge ukashindwa kumtumikia Mungu, kasapoti kazi ya Mungu kwa mapato tako, katafute muda wa kumwabudu Mungu pamoja na kutingwa ktk Biashara hiyo, ukijua siku utakapokufa biashara haitakuokoa.

✍🏾 Mfanyakazi ofisini kwako Bwana Mungu wa mbinguni akakuimarishe pamoja na changamoto zako, ukatafute kusudi la Mungu, wafanyakazi wezako na wateja wakajue Mungu wa mbinguni bado ana wafuasi wake waaminifu, usiruhusu chochote kile ktk kazi kiharibu uhusiano wako na Mungu. Kataa kutumiwa na shetani, hubiri hapo ulipo akiwemo hata bosi, _kataa mahubiri ya kishetani ya kukwambia huwezi au utaonekanaje_

✍🏾 Katika kazi nyingine, familia na chochote ufanyacho kaimarike zaidi pia, zidi kuwa imara  ktk kila jambo. Usikubali kuwa palepale. Kataa mahubiri ya shetani ya kukukatisha tamaa. *Kataa*tangu sasa. _Sema shetani hauwezi, nitazidi kuimarika katika Bwana nikiitenda kazi yake siku zote_

✍🏾 Maandiko hayo yanasema pia tusitikisike siku zote tukitenda kazi yako, ndugu mpendwa *_tusitikisike_*  *_tukaitende kazi yake siku zote_*. Najua kutikiswa kupo ila usikubali kutikiswa, hata km majaribu yako ni makali km moto, hata kama adui zako wamesimama kinyume nawe. Unajua nini, kikubwa hapa ni *usikubali kutikisika ingawa kutikiswa kupo* yaani hata km shetani atajaribu kukutikisa mwambie hivi _hivi unaweza kuitikisa ngome ya Yesu, mwambie toka lini we shetani ukamtikisa Mungu, asipo kujibu mwambie nipo ndani ya ngome imara isiyoweza kutikiswa na chochote_.

✍🏾 Ila yooote haya maandiko haya yanatufarijikwa kutuambia *kazi yetu si bure ktk Bwana*. Simama na usonge mbele, tutalipwa tusipozimia moyo, anasema hakuna atendaye kazi pasipo ujira.

By Isaac Lwendela: Mkristo
0768183433; 0783184333.
isaaclwendela@gmail.com.
📚UBARIKIWE EWE SHUJAA📚

No comments:

Post a Comment