KIU YA MUNGU NI WANADAMU WAMSIKIE
Kumbukumbu la Torati 4:7
Kwa maana liko taifa gani kubwa, lililo na Mungu aliye karibu nao, kama BWANA, Mungu wetu, alivyo, kila tumwitapo?
Ushawahi kujua kuwa Mungu atamani umsikie zaidi Yeye kuliko unavyotamani kumsikia?
Mungu wetu kila wakati anatamani tumsikie Yeye. Anatamani kila kitu tumwite Yeye. Anatamanj kwa kila alitendalo mwanadamu Yeye awe wa kwanza. Yeye awe tegemeo la kila kitu. Anatamani kutuponya lakini tumegeuza shingo zetu. Anatamani tuijue hii siri kuwa sisi tuliokolewa hatupaswi kuwa wanyonge maana ndani Yetu anaishi muumbaji wa Ulimwengu na mbingu.
Je ukiijua hii siri kuwa ndani yako yupo aliyeifanya hata misingi ya dunia, kipi cha kukutisha? Kipi cha kukuogifya? Je ni wachawi, wanganga? Hawa nao ni kazi ya mikono yake. Je ni shetani au mapepo au majini, hawa wote walikwisha kusetwa chini kabisa na kukanyagwa kwa ukuu na uweza wa jina la Yesu Kristo, zaidi ya yote Mungu amekupa nguvu na amri ya kukanyaga nguvu zote za yule adui.
Kama tumembeba ndani Mungu wetu, maana yake kwamba kila uonapo una haja, mwite Yeye, mwambie baba, hili linafanyikaje, lakini wakatu mwingine ni kutumia mamlaka ulinayo, kuuambia ugonjwa toka, kuiambia shida toka, kumwambia shetani toka. Nakumbuka juzijuzi nilijiskia kuumwa, nikajisema ndani ya moyo mimi siumwi maana ndani yangu anaishi aliyechukua magonjwa na madhaifu yangu yote. Baada ya masaa machache hali ya kuumwa ikatoweka.
Kwa hiyo kwa kule kuokoka na kufanywa mwana wa Mungu, haimanishi kuwa hali ngumu hazitakujia ila je una mtazamo gani uonapo hali tofauti, unapojisikia kuumwa, je mbele yako unaona nini panado au uzima? Unakimbilia hospital au unatamka nini.
Unapopitia katika changamoto unamshirikisha nani? Je unaumiza akili yako unamwambia Mungu aliye mkuu ndani yako?
Siku ya leo, mwite Mungu. Iambie kila hali ngumu kuwa wewe siyo mkuu kuliko Mungu. Uambie ugonjwa wewe una mamlaka gani ya kukaa ndani yangu, je haujui kuwa hapa hapana makao yako, haujui Yesu alishakuhamisha hapa? Iambie baishara yako, kuwa unaendeshwa kwa nguvu za aliyeiumba dunia, mwanafunzi yaambie masomo yako, ndani yangu ipo akili ya Mungu. Kila hali ngumu wewe mwite Mungu tu, Yeye yupo karibu zaidi ya ngozi yako.
Mamlaka haya ni dhahiri zaidi kwa waliompokea Kristo km Bwana na mwokozi wa maisha yao. Kwa ambayo hujapata neema hii, tuwasiliane inbox, siyo suala gumu.
By Isaac Lwendela; Redeemed.
0768183433; (whatsApp)
0783183433;
0679183438.
isaaclwendela@gmail.com
Facebook: mwl Isaac Lwendela
No comments:
Post a Comment