Saturday, 3 June 2017

MWALIKO WA YESU

MWALIKO WA YESU

Ufunuo 3:20

Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.

Ni sauti ya upendo na huruma, iliyojaa amani, neema, rehema na msahamaha. Ni sauti ya Yesu Kristo; akibisha hodi moyoni mwa mwanadamu, akitamani mwanadamu amskie hata sekunde moja, apate kumpa uzima, maana anajua bila Yeye hakuna mtu wa kupata uzima, bila Yeye ambaye ndiye njia ya kweli na uzima mwanadamu atapotelea jehanamu.

Unangoja nini kufungua mlango ili aje afanye makao kwako? Anasema atafanya makao ndani yako, atakula pamoja nawe, je si upendeleo mkuu kula pamoja na mfalme wa mbingu na dunia, kula na Mfalme wa wafalme, kuishi pamoja na Bwana wa mabwana.

Kuna rafiki huwa ananiambia, Isaac, hivi kama Mungu  yupo kwa nini kuna shida hizi, kwa nini alinirihusu nizaliwe mimi nisiyeamini. Huwa namwambia kutokuamini ni kazi ya shetani ambaye *hupofusha fikra za watu na kuzitia ganzi akili zao ili nuru ya wokovu isiwazukie*. Ila Mungu anatamani kila mwanadamu aokolewe, Mungu anasema hafurahii kifo cha mwenye dhambi. Kuhusu shida ni kwa sababu wewe hujaamua kumtwisha Yeye fadhaa zako zote, Maana anasema hakuna linalomshinda.

Wewe uliyeamini fungua tena mlango asubuhi ya leo, Mfalme wa amani atakupa amani ipitayo fahamu zote za wanadamu.

Mtwishe fadhaa zako zote, maana yeye hujishughulisha sana na mambo yako. Usitegemee akili zako. Ya nini kuhangaika na kusumbua akili zako wakati wajua huwezi hata kuongeza unywele mmoja katika kichwa chako?

Rafiki ambaye hujapata neema ya kuamini. Mlango upo wazi, fungua moyo wako, amua kumkubali leo hata kwa dhali uone yatakayotokea maishani mwako. Yeye atakusaheme dhambi zako *zooooote*, utafanyika kiumbe kipya, mtu mpya, mwana wa Mungu na mtakatifu.

Tafadhali usipoteze mwaliko huu. Unajua Yeye akiingia tu mambo yako yote lazima yanyooke, na kumbuka tupo katika siku za mwisho ambapo ulimwengu wote utahukumiwa, dhambi na mauti zitahukumiwa, dhambi zikiweo ndani yako nawe utakuwa sehemu ya ile hukumu. Tengeneza na Mungu leo.  Amua kumpokea leo.

By Isaac Lwendela; Redeemed.
0768183433; (WhatsApp)
0783183433;
0679183438.
isaaclwendela@gmail.com
Facebook, Mwl Isaac Lwendela

No comments:

Post a Comment