Saturday, 3 June 2017

YESU ALIKUJA AWAOKOE WENYE DHAMBI

YESU ALIKUJA AWAOKOE WENYE DHAMBI

1 Timotheo 1:15

Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi

Wanadamu wote tangu asili tuna dhambi, tumepungukiwa na utukufu wa Mungu. Hakuna mwanadamu mwenye haki hata mmoja. Mungu atakuja kuihukumu dhambi na mauti, je ni nani atakayepona wakati hakuna mwenye haki hata mmoja? Hakuna mwanadamu awezaye kujiokoa kwa juhudi zake, matendo mema hayawezi kukuokoa, kujitahidi kwako hakuwezi kukuokoa.

Lakini habari njema ni hii ya kuwa Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi hapa ndipo ulipo ukombozi wetu, kwamba mwenye dhambi aookolewe kupitia yeye. Yeye alibeba dhambi zote pale msalabani, aliteswa na kuonewa kwa ajili yetu, aliyabeba makosa yetu pale msalabani.

Kazi yako kubwa ni moja tu kuamini moyoni mwako ya kuwa alikuja duniani akateswa na kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zako, lakini siku akafufuliwa siku ya tatu, akapaa mbinguni, baada ya kuamini moyoni mwako, hatua inayofuata ni kukiri kwa kinywa chako na kuomba akusamehe na uwe kiumbe kipya.

Hapo ndipo utapokea haki yako, Mungu hatakulazimisha kuamini.

Wakati wa wokovu ni sasa, ya kesho huyajui. Na baada ya kifo ni hukumu. Mlango wazi karibu inbox.

Tuma ujumbe huu kwa ndugu jamaa na marafiki ambao hawajapata neema ya kumpokea Kristo.

By Isaac Lwendela; Redeemed.
0768183433; (WhatsApp)
0783183433;
0679183438.
Facebook Mwl Isaac Lwendela
isaaclwendela@gmail.com

No comments:

Post a Comment