Saturday, 3 June 2017

KWA NINI YESU TU?

KWA NINI YESU TU?

Kwa nini Yesu tu?

Wapo wengi waliozaliwa na wanawake lakin kuzaliwa kwa Yesu kulikuwa tofauti!

Wapo wengi waliotenda miujiza lakini miujiza ya Yesu ni aina yake na haina mfano wake, kumbuka miujiza ambayo Musa aliitenda, Eliya na Elisha!

Wapo wengi waliokufa lakin kifo cha Yesu ni cha tofauti ndo kiliturudishia mamlaka aliyokuwa ametulaghai shetani

Wapo wengi waliotundikwa msalabani lakini msalaba wa Yesu ndiyo nguvu ya waamini, ni ukombozi wa wanadamu, ni injili kamili!

Wapo wengi waliokufa na.kufufuka lakin ufufuo wa Yesu ni wa milele, na pia kwa ufufuo wake anatulisha kuwa miili yetu inapaswa kufufuliwa na naye!

Wapo wengi waliokuwa wana hekima lakini baada ya kufa kwao hekima yao inadumu kwa vitabu na makala mbalimbali lakn Yesu pekee ndiye hata mfupa haukuoza na bado anaishi na hekima yake ingali ktk kinywa chake!

Wapo manabii wengi sana waliopita lakin wengi wao bado hawakuwa wakamilifi km Yesu, mkumbuke nabii Isaya anasema kinywa changu ni kichafu n.k! Kumbula Musa, mkumbuke Daudi, Mkumbe Daniel anappsema nilipokuwa nikiungama dhambi yangu....! Mkumbe Ibrahim bado kuna mahali alidanganya, mkumbuke Paulo anappsema nakaza, mwendo, pia anasema naushulutisha mwili wangu ili nisiwe mtu wa kukataliwa! Ni Yesu pekee aliyesema ni nani anayenishuhudia kuwa nina dhambi!

Wapo walijaribiwa wakaanguka ktk dhambi, mfano, Adamu Daudi, Petro n.k ila ni Yesu pekee aliyeshinda kila majaribu ya shetani

Yapo mengi ya kujiuliza kuhusu Yesu but kumbuka kuwa aliyafanya hayo akiwa ni binadamu asilimia mia, akijaribu kutuonesha kuwa mtu aliyekombolewa kuwaje, mtu wa rohoni anapaswa kuwaje!

Yeye ndiye kielelezo halisi cha maisha ya Mkristo, tukishakombolewa tunakuwa viumbe wapya tuliozaliwa kwa jinsi ya rohoni, tunapokea tabia mpya za Kiungu huku tukiuvua utu wetu wa kale na kuvaa utu mpya wa Mungu ulioumbwa kwa ajili yetu!

Kumbuka alisema amwaminiye yeye atafanya makubwa kuliko aliyofanya Kristo! Bila shaka tunajua aliyoyafanya Kristo, ni mengi mno! Na anataka tufanye zaidi sisi tunaomwamini! Tujifunze kwake, tuisikie sauti yake, ninaamini anazangumza nasi siku zote akituelekeza ya kufanya ila masikio yetu ndiyo mazito, tumwombe Mungu atufungue kwa kuisikia sauti yake, je umepokea ujazo wa Roho Mtakatifu? Huyu ndiye mwalimu wetu, kiongozi wetu, msaidiz wetu, mfariji wetu na mpashaji wa yote yatolewayo na kinywa cha Kristo! Ndiye mfufuaji wa miili yetu iliyo ktk hatari ya kufa na ndiye alimfufua Kristo! Tuna nguvu hii ya Roho Mtakatifu ndani yetu km tumempokea!

Unapoendelea kutafakari kwa nini Yesu Kristo, hebu tafakari tena kwa nini naitwa Mkristo (yaani kwa nn usijiite mpagani)? na pia jiulize mpagani ni nani?

By Isaac Lwendela; Mkristo

KIU YA MUNGU NI WANADAMU WAMSIKIE

KIU YA MUNGU NI WANADAMU WAMSIKIE

Kumbukumbu la Torati 4:7

Kwa maana liko taifa gani kubwa, lililo na Mungu aliye karibu nao, kama BWANA, Mungu wetu, alivyo, kila tumwitapo?

Ushawahi kujua kuwa Mungu atamani umsikie zaidi Yeye kuliko unavyotamani kumsikia?

Mungu wetu kila wakati anatamani tumsikie Yeye. Anatamani kila kitu tumwite Yeye. Anatamanj kwa kila alitendalo mwanadamu Yeye awe wa kwanza. Yeye awe tegemeo la kila kitu. Anatamani kutuponya lakini tumegeuza shingo zetu. Anatamani tuijue hii siri kuwa sisi tuliokolewa hatupaswi kuwa wanyonge maana ndani Yetu anaishi muumbaji wa Ulimwengu na mbingu.

Je ukiijua hii siri kuwa ndani yako yupo aliyeifanya hata misingi ya dunia, kipi cha kukutisha? Kipi cha kukuogifya? Je ni wachawi, wanganga? Hawa nao ni kazi ya mikono yake. Je ni shetani au mapepo au majini, hawa wote walikwisha kusetwa chini kabisa na kukanyagwa kwa ukuu na uweza wa jina la Yesu Kristo, zaidi ya yote Mungu amekupa nguvu na amri ya kukanyaga nguvu zote za yule adui.

Kama tumembeba ndani Mungu wetu, maana yake kwamba kila uonapo una haja, mwite Yeye, mwambie baba, hili linafanyikaje, lakini wakatu mwingine ni kutumia mamlaka ulinayo, kuuambia ugonjwa toka, kuiambia shida toka, kumwambia shetani toka. Nakumbuka juzijuzi nilijiskia kuumwa, nikajisema ndani ya moyo mimi siumwi maana ndani yangu anaishi aliyechukua magonjwa na madhaifu yangu yote. Baada ya masaa machache hali ya kuumwa ikatoweka.

Kwa hiyo kwa kule kuokoka na kufanywa mwana wa Mungu, haimanishi kuwa hali ngumu hazitakujia ila je una mtazamo gani uonapo hali tofauti, unapojisikia kuumwa, je mbele yako unaona nini panado au uzima? Unakimbilia hospital au unatamka nini.

Unapopitia katika changamoto unamshirikisha nani? Je unaumiza akili yako unamwambia Mungu aliye mkuu ndani yako?

Siku ya leo, mwite Mungu. Iambie kila hali ngumu kuwa wewe siyo mkuu kuliko Mungu. Uambie ugonjwa wewe una mamlaka gani ya kukaa ndani yangu, je haujui kuwa hapa hapana makao yako, haujui Yesu alishakuhamisha hapa? Iambie baishara yako, kuwa unaendeshwa kwa nguvu za aliyeiumba dunia, mwanafunzi yaambie masomo yako, ndani yangu ipo akili ya Mungu. Kila hali ngumu wewe mwite Mungu tu, Yeye yupo karibu zaidi ya ngozi yako.

Mamlaka haya ni dhahiri zaidi kwa waliompokea Kristo km Bwana na mwokozi wa maisha yao. Kwa ambayo hujapata neema hii, tuwasiliane inbox, siyo suala gumu.

By Isaac Lwendela; Redeemed.
0768183433; (whatsApp)
0783183433;
0679183438.
isaaclwendela@gmail.com
Facebook: mwl Isaac Lwendela

MWALIKO WA YESU

MWALIKO WA YESU

Ufunuo 3:20

Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.

Ni sauti ya upendo na huruma, iliyojaa amani, neema, rehema na msahamaha. Ni sauti ya Yesu Kristo; akibisha hodi moyoni mwa mwanadamu, akitamani mwanadamu amskie hata sekunde moja, apate kumpa uzima, maana anajua bila Yeye hakuna mtu wa kupata uzima, bila Yeye ambaye ndiye njia ya kweli na uzima mwanadamu atapotelea jehanamu.

Unangoja nini kufungua mlango ili aje afanye makao kwako? Anasema atafanya makao ndani yako, atakula pamoja nawe, je si upendeleo mkuu kula pamoja na mfalme wa mbingu na dunia, kula na Mfalme wa wafalme, kuishi pamoja na Bwana wa mabwana.

Kuna rafiki huwa ananiambia, Isaac, hivi kama Mungu  yupo kwa nini kuna shida hizi, kwa nini alinirihusu nizaliwe mimi nisiyeamini. Huwa namwambia kutokuamini ni kazi ya shetani ambaye *hupofusha fikra za watu na kuzitia ganzi akili zao ili nuru ya wokovu isiwazukie*. Ila Mungu anatamani kila mwanadamu aokolewe, Mungu anasema hafurahii kifo cha mwenye dhambi. Kuhusu shida ni kwa sababu wewe hujaamua kumtwisha Yeye fadhaa zako zote, Maana anasema hakuna linalomshinda.

Wewe uliyeamini fungua tena mlango asubuhi ya leo, Mfalme wa amani atakupa amani ipitayo fahamu zote za wanadamu.

Mtwishe fadhaa zako zote, maana yeye hujishughulisha sana na mambo yako. Usitegemee akili zako. Ya nini kuhangaika na kusumbua akili zako wakati wajua huwezi hata kuongeza unywele mmoja katika kichwa chako?

Rafiki ambaye hujapata neema ya kuamini. Mlango upo wazi, fungua moyo wako, amua kumkubali leo hata kwa dhali uone yatakayotokea maishani mwako. Yeye atakusaheme dhambi zako *zooooote*, utafanyika kiumbe kipya, mtu mpya, mwana wa Mungu na mtakatifu.

Tafadhali usipoteze mwaliko huu. Unajua Yeye akiingia tu mambo yako yote lazima yanyooke, na kumbuka tupo katika siku za mwisho ambapo ulimwengu wote utahukumiwa, dhambi na mauti zitahukumiwa, dhambi zikiweo ndani yako nawe utakuwa sehemu ya ile hukumu. Tengeneza na Mungu leo.  Amua kumpokea leo.

By Isaac Lwendela; Redeemed.
0768183433; (WhatsApp)
0783183433;
0679183438.
isaaclwendela@gmail.com
Facebook, Mwl Isaac Lwendela

YESU ALIKUJA AWAOKOE WENYE DHAMBI

YESU ALIKUJA AWAOKOE WENYE DHAMBI

1 Timotheo 1:15

Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi

Wanadamu wote tangu asili tuna dhambi, tumepungukiwa na utukufu wa Mungu. Hakuna mwanadamu mwenye haki hata mmoja. Mungu atakuja kuihukumu dhambi na mauti, je ni nani atakayepona wakati hakuna mwenye haki hata mmoja? Hakuna mwanadamu awezaye kujiokoa kwa juhudi zake, matendo mema hayawezi kukuokoa, kujitahidi kwako hakuwezi kukuokoa.

Lakini habari njema ni hii ya kuwa Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi hapa ndipo ulipo ukombozi wetu, kwamba mwenye dhambi aookolewe kupitia yeye. Yeye alibeba dhambi zote pale msalabani, aliteswa na kuonewa kwa ajili yetu, aliyabeba makosa yetu pale msalabani.

Kazi yako kubwa ni moja tu kuamini moyoni mwako ya kuwa alikuja duniani akateswa na kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zako, lakini siku akafufuliwa siku ya tatu, akapaa mbinguni, baada ya kuamini moyoni mwako, hatua inayofuata ni kukiri kwa kinywa chako na kuomba akusamehe na uwe kiumbe kipya.

Hapo ndipo utapokea haki yako, Mungu hatakulazimisha kuamini.

Wakati wa wokovu ni sasa, ya kesho huyajui. Na baada ya kifo ni hukumu. Mlango wazi karibu inbox.

Tuma ujumbe huu kwa ndugu jamaa na marafiki ambao hawajapata neema ya kumpokea Kristo.

By Isaac Lwendela; Redeemed.
0768183433; (WhatsApp)
0783183433;
0679183438.
Facebook Mwl Isaac Lwendela
isaaclwendela@gmail.com

VITA NI VYA BWANA

VITA NI VYA BWANA.

2 Nyakati 20:15,17

..........na wewe mfalme Yehoshafati; BWANA awaambia hivi, *Msiogope, wala msifadhaike kwa ajili ya jeshi kubwa hili; *_kwani vita si yenu bali ni ya Mungu._*

17 Hamtahitaji kupigana vita jipangeni, simameni, mkauone wokovu wa BWANA ulio pamoja nanyi,_ enyi Yuda na Yerusalemu; msiogope, wala msifadhaike; kesho tokeni juu yao; kwa kuwa BWANA yu pamoja nanyi.

Wakati mwingi sana katika maisha tumekuwa tukipambana na changamoto za maisha kwa kutumia nguvu zetu wenyewe.

Lakini kwa ambao tumemchagua Yesu Kristo kuwa kiongozi wa maisha yetu wa maisha yetu haipaswi kuwa hivyo.

Yeye ndiye Bwana wa vita vyetu, vita vyetu ni vyake Yeye wala siyo vyetu.

Changamoto ulizonazo, iwe ni madeni, familia, uchumi mgumu, masomo magumu, kuteswa na adui, magonjwa, shida, tatizo la ajira, tambua kuwa kama Yesu Kristo ni kiongozi wa maisha yako, hizo shida zote ni za Bwana. Kazi yako kubwa ni kumtwisha fadhaha zako zote.

Usijisumbue neno lolote bali kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru (Filipi 4:6). Mtwishe fadhaa zako zote na mizigo yako, naye atakumpuzisha.

Wakati wa shida na majaribu mazito kama ya mfalme Yehoshafati, wewe msifu Mungu, liamini neno lake, nenda mbele zake kwa kuomba. Hivi ndivyo walivyofanya mashahidi waliotutangulia kama akina Paulo na SIla, mwisho milango ya gereza ikafunguka, minyororo ikafunguka na kila namna ya kifungo kikaachia wakawa huru.

Inuka ewe shujaa kama Gideoni, simama umsifu Mungu ewe uliye kwenye kifungo kama Paulo, nenda mbele za Mungu na umsifu Bwana kama Yehoshafati alitangaziwa vita na badaye adui wakauwana wao kwa wao.

Vita ni vya Bwana, aliye ndani yetu ni mkuu kuliko yeyote duniani na mbinguni na ndiye Bwana wa vita. Mwite Yeye, atakushangaza, atakupigania, atakufanikisha mwaka huu.

USIOGOPE.
INUKA EWE SHUJAA.
MWENYE KUSHINDA ZAIDI YA KUSHINDA.
MWANA WA MFALME.
SIMAMA UMILIKI NA KUTAWALA.
By Isaac Lwendela: Mkristo.
isaaclwendela@gmail.com
0768183433/0679183438.

UJANA WAKO

UJANA WAKO UNADHAURIKA KWA LIPI?

1 Timotheo 4:12
Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.

Katika nyakati za leo, vijana wamekuwa hawaaminiki katika kanisa wanaonekana wapenda usasa, wapenda dunia kuliko Mungu, wapapalikaji wa huduma na mengine.

Katika baishara wanaonekana matapeli, wapiga dili, wasioaminika, wanapenda njia za panya zaidi kufikia mafanikio na mengine mengi.

Katika kazi, makapuni na taasisi nyingi zimetokea kutokuwaamini vijana kwa sababu ya *wavivu, wachelewaji, wanapenda mapenzi kuliko kazi, wanapenda zaidi kuchati kuliko kazi yenyewe huku wakitegemea kupandishwa cheo, bonus na promotion.

Katika shule na vyuoni, vijana wajanya ni wale wazee wa mitoko, fashion za kila namna, misimu mikubwa kubwa, mapenzi kwa sana na starehe za kila namna, wakija mtaani mambo yanakuwa kinyume kabisa.

Vijana wapenda ajira kuliko kutengeneza ajira.

Vijana wenye kujiharibu kwa madawa ya kulevya, ngono, ukahaba, kuuza miili yao. Wasijue wapewa zamu moja tu duniani kuishi.

Vijana walio jaa matusi ya kila namna, lawama kwa serikali huku wakishinda vijiweni.

Kijana mwezangu utakuwa baba wa namna wa gani? Ewe binti utakuwa mama wa namna gani? Wa kuonesha maungu yako kwa watoto wako?

Je tutajenga taifa la namna gani? Nini hatima yako?

Kwa mambo hayo kwa nini ujana wetu usidharauriwe?

Kesho yako inaandaliwa na ujana wako wa leo. Unafanya sasa ni matunda ya kesho.

Kuwa mfano katika *usemi wako, kila ufanyalo, tabia, upendo, imani na usafi*

#Inuka ewe kijana mwenye nguvu.
#Ukajenge taifa na kuangaza
#Ukawe mfano wa kuigwa.

By Isaac Lwendela.
0768183433, 0679183438, 0783183433.
isaaclwendela@gmail.com.

Tuesday, 14 June 2016

MLANGO WA KUFAA, UNAOPINGWA

*MLANGO WA KUFAA, UNAOPINGWA*

*1 Wakorintho 16:9*
 *_kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wako wengi wanipingao_*

Hayo yalikuwa ni maneno Paulo akinena juu ya nafasi ya kuhubiri aliyekuwa amepewa jiji la Efeso. Lakini pamoja na kufunguliwa mlango huu wa kufaa wapo walioinuka kumpinga na si wachache, tazama Matendo 19:13 na kuendelea, utaona namna alivyopingwa.

✍๐ŸพMlango ni fursa ya kufanya kitu fulani, ni kibali, nafasi. Ni opportunity ya kufanya jambo fulani.

✍๐Ÿพ Kuna fusra nyingi ambazo tunazo hasa baada ya kuokoka, tofauti na walimwengu. Ipo milango mikubwa sana ya baraka ambayo tayari tumefunguliwa. Tena ya kufaa sana.

✍๐Ÿพ Yawezekana umefunguliwa mlango wa kufaa katika huduma za kuhubiri, kufundisha neno la Mungu, kuwatia moyo watu, kuwasaidia watu, kukirimu, kulijenga kanisa la Mungu kiroho. Lakini wapo wapingao huduma hizo.

✍๐Ÿพ Yawezekana umepata Mlango wa kufaa katika katika biashara, kilimo, biashara, kazi yako, Elimu yako, familia yako au chochote kile ambacho kuna fursa, ila wapo wapingao, vipo vizuizi vikubwa sana.

✍๐Ÿพ Hao wapingao au hivyo vikwazo havisababishwi na watu wa kazini kwako, rafiki zako, wazazi wako, wachungaji wako au washindani wako ila ni ibilisi awatumiaye kuziba huo mlango, yeye ndiye huwatumia kuleta vikwazo na kupinga kwa namna yoyote ile ili usifanikiwe. Hutumia mapepo ili kuharibu huo mlango.

✍๐Ÿพ Kazi yetu leo ni moja, ni kuwapinga na wale watupingao kwa Damu ya Yesu Kristo wa Nazareti _*nao wakamshinda kwa damu ya Mwanakondooo*      (Ufunuo 12:11). Kuwapiga wale wazibao na kuweka vizuizi ktk milango yetu, _*mpingeni shetani naye atawakimbia,  (Yakobo 4:7)*_

✍๐Ÿพ Shetani ndiye apingaye na kuzuia mafanikio yetu, _*milango yetu ya masomo, milango ya huduma, milango ya biashara, milango ya baraka tele, milango ya uponyaji, yeye ndiye anayezuia uponyaji na kutesa watu, yeye ndiye mkatishaji tamaa, mtia woga kwa watu, mvuruga ndoa*_.

✍๐Ÿพ Maadam tumejua haki yetu kuwa tunayo, kuwa tuna milango iliyo wazi ila inazuiwa na huyu aliyeshindwa, tutasimama na kumwendea kwa jina la Bwana kama Daudi alivyomwendea Goliathi, tutakata kichwa chake na kuwapa ndege wale, tumechoka huyu mwovu kuyatukana majeshi ya Bwana, maana wewe ni askari na familia ya Kristo lazima tuinuke na kushika nafasi zetu.

✍๐ŸพHata kama mlango wa kupata kazi au ajira unapingwa kuzuiwa, lakini ayefungua milango ya gereza, alikata minyororo ya Paulo na mapingu yupo sasa kuondoa vikwazo na makufuli na vitasa vya bandia alivyoweka shetani, maana ukiona mlango km umefungwa ujue ni kitasa au kufuli la bandia alimeliweka shetani, we tikisa kidogo na fungua ingia kwa jina la Yesu. Bwana atafungua milango ya kufaa ya kila namna kwa kadiri ya wito wako na kusudi lako ambalo ndo hapa duniani kwa ajili ya kulitimiza.

✍๐Ÿพ Kumbuka,  *_hautainuka na kumpinga huyu mpinzani na mzuiaji wa mlango wako bila silaha za Kiroho ambazo ni Neno la Mungu, Imani, sala, maombi, utayari wa huduma, haki na utakatifu, lazima ujikane, ujitenge na tamaa za dunia hii, kujitenga na walimwengu, na kuukataa uovu kwa gharama yoyote ile, hata kumwagika damu ( Waebrania 12:4) inasema hamjafanya vita hata kumwagika damu,  mkishindana na dhambi_*

✍๐Ÿพ INUKA MPENDWA, HATUNA MJI UDUMUO HAPA. Jikane na ujitwike Msalaba wake, hapo utaona haya yakitimia, utaona pingu za shetani ktk milango yako ya mafanikio ikifunguka. Kumbuka haufanyi chochote ila kupata baraka zaidi ya kumpa moyo wako Kristo, na kulikubali kulitii neno lake.

By Isaac Lwendela; Mkristo
0768183433; 0783184333.
isaaclwendela@gmail.com