VITA NI VYA BWANA.
2 Nyakati 20:15,17
..........na wewe mfalme Yehoshafati; BWANA awaambia hivi, *Msiogope, wala msifadhaike kwa ajili ya jeshi kubwa hili; *_kwani vita si yenu bali ni ya Mungu._*
17 Hamtahitaji kupigana vita jipangeni, simameni, mkauone wokovu wa BWANA ulio pamoja nanyi,_ enyi Yuda na Yerusalemu; msiogope, wala msifadhaike; kesho tokeni juu yao; kwa kuwa BWANA yu pamoja nanyi.
Wakati mwingi sana katika maisha tumekuwa tukipambana na changamoto za maisha kwa kutumia nguvu zetu wenyewe.
Lakini kwa ambao tumemchagua Yesu Kristo kuwa kiongozi wa maisha yetu wa maisha yetu haipaswi kuwa hivyo.
Yeye ndiye Bwana wa vita vyetu, vita vyetu ni vyake Yeye wala siyo vyetu.
Changamoto ulizonazo, iwe ni madeni, familia, uchumi mgumu, masomo magumu, kuteswa na adui, magonjwa, shida, tatizo la ajira, tambua kuwa kama Yesu Kristo ni kiongozi wa maisha yako, hizo shida zote ni za Bwana. Kazi yako kubwa ni kumtwisha fadhaha zako zote.
Usijisumbue neno lolote bali kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru (Filipi 4:6). Mtwishe fadhaa zako zote na mizigo yako, naye atakumpuzisha.
Wakati wa shida na majaribu mazito kama ya mfalme Yehoshafati, wewe msifu Mungu, liamini neno lake, nenda mbele zake kwa kuomba. Hivi ndivyo walivyofanya mashahidi waliotutangulia kama akina Paulo na SIla, mwisho milango ya gereza ikafunguka, minyororo ikafunguka na kila namna ya kifungo kikaachia wakawa huru.
Inuka ewe shujaa kama Gideoni, simama umsifu Mungu ewe uliye kwenye kifungo kama Paulo, nenda mbele za Mungu na umsifu Bwana kama Yehoshafati alitangaziwa vita na badaye adui wakauwana wao kwa wao.
Vita ni vya Bwana, aliye ndani yetu ni mkuu kuliko yeyote duniani na mbinguni na ndiye Bwana wa vita. Mwite Yeye, atakushangaza, atakupigania, atakufanikisha mwaka huu.
USIOGOPE.
INUKA EWE SHUJAA.
MWENYE KUSHINDA ZAIDI YA KUSHINDA.
MWANA WA MFALME.
SIMAMA UMILIKI NA KUTAWALA.
By Isaac Lwendela: Mkristo.
isaaclwendela@gmail.com
0768183433/0679183438.
This is heartwarming.
ReplyDeleteBarikiwa Mtumishi. Kweli vita si vyetu Bali ni Bwana.
ReplyDeleteHakika nimeinuka Tena
ReplyDelete